Pages

Ads 468x60px

I'm upcoming Dj in The music Industry this is my free Blog where I can share my Ideas to the World.

Sunday, January 6, 2013

STAMINA FT. MAVOKO - NAJUTA LYRICS

SONG: NAJUTA
ARTISTS: STAMINA FT RICH MAVOKO
PRODUCER: KEVY
STUDIO: SNAP RECORDS
SONG WRITER: STAMINA & RICH MAVOKO
SONG DURATION: 03:50

INTRO
Rich mavoko:uoooooooooooooooooooooannnnnhhhhaaa{x3}
Stamina;izmoro town baby,imback,u know watkevy,thisiz so matured meeeen

Vers 1{stamina}
Shida zinaomba urafiki,umasikini unaleta posa
Ukubwa meli ya kigiriki,nimezamia bila boxer
Bikra ya utoto,imeshavunjwa na balehe
Ukubwa una mingi misoto,namchanganyo wa starehe
Mara ooooh baba kijacho,etiniandae hela ya nepi
Wife anatoa macho,anangoja shopping ya sketi
Hakimu ananyundo ya noti,mtuhumiwa nasaka chenchi
Bongo mahakama za joti,me mpoki nabaki benchi
Hata nikimchukia baniani,kiatu chake kina mchango
Mzinzi na nyotaya kijani,ndio uzazi usiokua na mpango
Balehe noma,kama baunsa aliyepigwa na mtoto
Ukubwa mechi ya kisodoma,haiwezichezeshwa na mpoto
Aaaaahkas na kas,ni kasi isiyokua na kasi
Ila nikiweka kas na kus,ndio kusi pacha wa kasi
Bora wewe jalala,me ukubwa shimo la choo
Ukichanganya na ufukara,ndio mechii siyokua na droo

Choruss{rich mavoko}
Kama nakufuru,Mungu naomba unisamehe
Nakosa uhuru,sikumbuki hata tarehe
Kweli najutakuzi jua hizi stareheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeehh
Ehhhh me najuta kubalehe
Ehhhh sikumbuki hata tarehe
Eeee ujana maji ya moto,zinaniunguza hizi starehe

Vers 2{stamina}
Maisha ngumi ya bitozi,siogopi kutega sura
Pesa sitafuti kwa pozi,bado najinyima kula
Nishachoka kusadiki,tomaso tangu na tangu
Marafiki wanafiki,wana snitch hadi kwa mke wangu
Majukumu ya familia,nimeyabeba bila ngata
Asili zimezidi mila,desturi zimenikamata
Haya maumivu ya mjeledi,kwenye ngozi ya mlemavu
Ukubwa mechi ya mabaamedi,me mlevi nafungwa kavu
Aaaah maisha jabali,ugomvi wa cheka na Tyson
Siku hizi ukinunua hata kagari,kitaani unaitwa free mason
Maumivu ya sufuria,jikoni hayana ushuru
Pesa tajiri wa dunia,mwenye hisa yangu ya uhuru
Aiseh sayansi imenikera,ukuaji umenipa msoto
Utu uzima bila hela,utamwa mkiahadi mtoto
Napopata mkwanja,nashida zinagonga hodi
Vipi nitanunua kiwanja,huku bado nadaiwa kodi

Choruss{rich mavoko}
Kama nakufuru,Mungu naomba unisamehe
Nakosa uhuru,sikumbuki hata tarehe
Kweli najutakuzi jua hizi stareheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeehh
Ehhhh me najuta kubalehe
Ehhhh sikumbuki hata tarehe
Eeee ujana maji ya moto,zinaniunguza hizi starehe

Vers 3{stamina}
Ukubwa msafara wa kenge,me mjusi vipi unichoshe
Penzi kitovu cha uzembe,nakaza nisiitwe ngoswe
Ugangstar bila hela,majibu yake ni uchafu
Maisha ya bongo msosi wa jela,so mfungwa usiulizie ndafu
Nilizoea kashata,bumunda na vibagia
Huku unga,bangi,nabapa,ndio vitu navyovisikia
Chuki na fitina,hadhina za wenye wivu
Wapo wanaonishirikina,ili moto nigeuke jivu
Udogoni nilidekezwa,wazazi walinipamalezi
Pesa imesomea udereva,inaendesha hadi mapenzi
Elimu ya njia za panya,inanikosesha michongo
Madeni yananiandama,kama serikali ya bongo
Maishani ukiwa govinda,wenzako watakuita yaya
Pesa mnyama anayewindwa,na jangiri aliyevuta kaya
Uwazi unanidondosha,bado narushiwakombora
Condom ndio kinga tosha,sijikingi na bastora

Choruss{rich mavoko}
Kama nakufuru,Mungu naomba unisamehe
Nakosa uhuru,sikumbuki hata tarehe
Kweli najutakuzi jua hizi stareheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeehh
Ehhhh me najuta kubalehe
Ehhhh sikumbuki hata tarehe
Eeee ujana maji ya moto,zinaniunguza hizi starehe

Bridge{rich mavoko}
Heri ni ngerudi utoto,ujana maji ya moto
Eeeeeeeeheeeeeheeeeeeeheeeeeeeehhh
Me najuta kubalehe,me najuta kubaleheeeeeeeh,me najuta kubaleeeeeeeeeeeeeehhhhhhhhh

Ontro{stamina}
Moro in da house,in da house
Moro town in da house,stamina in da house
Moro town in da house,stamina in da house
Ahahaha I luv hip hop



0 comments:

Post a Comment