Story ndie mtoto aliyeimba kiitikio katika wimbo wa Roma Mkatoriki wa
2030, ni mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 6 lakini ameonesha kipaji
ambacho kitakuja kuwa tishio apo baadae.
Baba mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa alikigundua kipaji cha mtoto wake
tangu akiwa na umri wa miaka mitatu kwani kila akiweka muziki anaamuona
mtoto wake anafatilisha na kuimba vizuri, shuleni pia alikuwa kwenye
kikundi cha kuimba na alipata nafasi ya kuimba siku ya 'Mtoto wa Afrika'
ambapo alifanya vizuri,.
Alisema mwanae anapenda sana kuimba nyimbo ya Joti "Husomeki' na nyimbo za Willow Smith.
Story anatarajia kuanza darasa la kwanza mwezi huu..
0 comments:
Post a Comment